HESLB KUENDELEA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO KUANZIA OKTOBA MOSI HADI OKTOBA 5

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa muda wa siku 5 kuanzia Oktoba mosi hadi 5 mwaka huu ili kuwawezesha wanafunzi waliomaliza mafunzo ya JKT hivi karibuni, kuingia katika mfumo wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao na kukamilisha maombi yao.

Aidha Kwa muda hui wa siku tano , mfumo utakuwa wazi ili kuwaruhusu waombaji amabao maombi yao yana mapungufu kurekebisha na kuweka nyaraka sahihi ili kuiwezesha HESLB kuendelea   na hatua nyingine.