UMATHSNET ni mtandao ulioanzishwa na Ndugu USMAN MCHINJA.(Mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Elimu na Hesabu Na TEHAMA.)

Kwa kutambua kuwa sasa tupo katika karne ya 21 ya Sayansi na Teknolojia , Mwalimu MCHINJA aliona iko haja ya kuanzisha mtandao utakaoweza kuwafanya wanafunzi wa kitanzania kujikwamua na kufika mbali kimaendeleo haswa kupitia HESABU Na TEHAMA.

UMATHSNET imejiwekea  malengo kadhaa ikiwemo kutoa elimu ya kutosha juu ya maswala mbali mbali ya kitaaluma, kusaidia wanafunzi wa ngazi ya chekechea, shule ya msingi, sekondari , elimu ya kati na elimu ya juu vile vile ili kuwawezesha kuongeza ufaulu katika masomo ya Hesabu na TEHAMA vile vile.

UMATHSNET imejikita zaidi katika kufanya tafiti juu ya njia bora zitakazowezesha ufundishwaji mzuri wa masomo ya HESABU na TEHAMA kwa ngazi ya  elimu ya msingi, sekondari, elimu ya kati na juu. 

Kupitia mtandao huu mwanafunzi ataweza kunufaika na maswali, majibu, majaribio mbalimbali , notisi za hesabu na TEHAMA, mada zilizoandaliwa na wataalamu mbalimbali kwa mfumo wa video, audio, PPT, PDF na vitabu vya kila aina.