Na Mwalim Usman Mchinja.

Hivi karibuni nimekuwa nikipokea simu na jumbe nyingi kutoka kwa Wazazi mbalimbali na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na Masomo ya Stashahada. Katika simu nilizokuwa nikipokea niliweza kuzigawa katika makundi mawili,.

Kundi la kwanza ni la wanafunzi au wazazi ambao hawajui kabisa nini wakifanye ili kuhakiki vyeti vyao.

kundi la pili lilikuwa la wazazi na wanafunzi waliokuwa wamefanya maombi hayo huku wakilalamika kuwa hadi sasa hawajapata majibu ya maombi yao.

Katika uchunguzi wangu , nilifanikiwa kugundua baadhi ya mambo ya msingi kabisa , na kwa andiko langu nitakwenda kuelezea kwa upande wa wanafunzi.

Katika simu zote nilizopokea na mwanafunzi kuniambia kuwa alifanya maombi ila hadi sasa hajapata majibu, swali langu la pili kumuuliza lilikuwa, je amefanya maombi hayo lini, kwa maana ya kuwa, zimepita siku ngapi hadi leo, kiasi cha kusema kuwa ni muda mrefu majibu yake yamechelewa sana. Idadi kubwa ilionesha wamefanya maombi muda wa Zaidi ya wiki moja.

Kwa kumsikiliza mwanafunzi kama huyu, ninachofanya ninamuomba ridhaa yake aniruhusu niingie kwenye mfumo aliotumia kufanya maombi hayo ili walau nijionee kuhusu aliyoyasema. Mara baada ya kunipatia username na password, na kufanikiwa kuingia kwenye mfumo, ndipo ninapofanya udadisi na kunyumbua mambo kadhaa ambayo wanafunzi wengi wanakosea na hata pasina kujua kuwa mambo hayo ndio yatakomfanya aidha achelewe kupata majibu yake kwa wakati au asipate majibu yeyote.

MAKOSA MATATU

Katika udadisi wangu kuna makosa matatu ambayo nimegundua wanafunzi wengu hufanya

1. KUFUNGUA AKAUNTI BILA KUFANYA MAOMBI YEYOTE

Sababu: Ndugu zangu, kwa kiasi kikubwa wanafunzi hawa ni wale ambao waliomba kusaidiwa kufanya maombi na hawakufuatilia kutaka kujua ni nini kimeombwa, kimeombwa wapi na kimeombwa vipi ili wakati wa majibu basi aweze kuyapata kwa wakati.

Hasara: Kundi hili RITA huwa haliwatambui kwani hakuna ombi lolote litakuwa limewasilishwa kwao.

Suluhu: Mwanafunzi ni wajibu wako kujua kila kitu kinachohusu maombi yako kwenye mfumo wa maombi wowote ule. Endapo utasaidiwa kufanya maombi, hakikisha unamuomba huyo aliyekusaidia kuomba akupatie username na password ili nawe uhakikishe kuwa ombi lako limeombwa kikamilifu.

2. KUFANYA MAOMBI BILA KUAMBATANISHA VYETI

Sababu: Kundi hili ni la wanafunzi ambao wanafanya maombi lakini wanasahau kuambatanisha vyeti , inawezekana kwa kusahau au pengine kwa kutokujua.

Hasara: RITA watapokea ombi lako lakini watashindwa kufanya maamuzi yeyote kwani hujaweka cheti ili wakithibitishe kuwa ni halisi au ni feki

Suluhu: Hakikisha kila unapofanya uhakiki, kabla haujalipia, hakikisha unapakia cheti chaki cha kuzaliwa kisha ulipie ndio ujue kuwa ombi lako limefika RITA na litafanyiwa kazi.

3. KUFANYA MAOMBI BILA KUFANYA MALIPO

Sababu: Hili hutokea kwa wanafunzi wengi haswa wakimkabidhi mtu asiyefahamu jinsi ya kuomba maombi hayo na kutokujua kuwa bila kulipia Tshs. 3000 kwa kila cheti maombi yatakuwa hayajakamilika.

Hasara: Ombi lako litafika RITA lakini halitofanyiwa kazi, hivyo utasuburia mda mrefu bila jitihada zako kuzaa  matunda.

Suluhu: Hakikisha kila ombi la uhakiki liambatane na malipo yake ya Tsh, 3000 kama control No. itakavyokuwa inaeleza.

Ndugu zangu, Mambo hayo matatu yakifanyiwa kazi basi angalau utakuwa na uhakika kuwa ombi lako limefika RITA na litakuwa linafanyiwa kazi.

Kwa kutambua hilo MANSAM SCHOLARS tumetengeneza mfumo rafiki kwa kila mmoja ,mrahisi kabisa kutumia ambapo mwanafunzi ataweza kuandika taarifa zake za muhimu ili kufanikisha maombi hayo , kisha timu ya wataalamu wenye uzoefu mkubwa watapokea taarifa zake na kumsaidia kufanya maombi hayo kwa umakini mkubwa sana na hatimaye kukamilisha maombi hayo. Kwa ambao hatakuwa na simu janja, basi atapiga tu simu kupitia 0655 258012 kisha atasikizwa na kusaidiwa.

Kupitia MANSAM  SCHOLARS mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kufuatilia na kuona kila hatua ambayo maombi yake yamefikia hadi pale yanapokuwa yamekamilika na majibu kurejeshwa ataweza kuyaona kupitia dashboard yake papo kwa papo akiwa popote nchini.

Huduma zetu zinapatikana Muda wote kupitia mfumo wetu unaopatikana kwenye tovuti ya  https://www.umathsnet.or.tz/MAMS/ .

MANSAM SCHOLARS imekusudia kusaidia kukamilisha furaha yako kupitia maombi mbalimbali.

Karibuni sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *